Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2023

Kwa nini Mazingira ni Uhai?

Picha
Tunapaswa kutunza mazingira yetu kwa sababu kilimo, ufugaji mvua, n.k. huathiriwa na uchafuzi wa mazingira

Kwanini Maporomoko ya Kalambo yanatajwa kuwa maajabu ya Afrika yaliyofic...

Picha
Hifadhi ya mazingira ni juhudi zinazofanywa na binadamu ili kuhakikisha ulimwengu anamoishi usiharibiwe na utendaji wake, bali uweze kuwafaa watu wa vizazi vijavyo. @mazingiratv5700 @ChanyATV @habutv33 @ortamisemi

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIWA KWENYE MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA MAFUTA YA TAIFA YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU (UAE) ENOC LLC, BW. SAIF AL FALASI ALIYEAMBATANA NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR TAREHE 28 JANUARI, 2023.

Picha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ENOC LLC, Bw. Saif Al Falasi aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Januari, 2023.  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Nishati tarehe 27 Januari, 2023 walisaini Mkataba wa makubaliano (Memorandum of Understanding) na Kampuni hiyo ya ENOC LLC kuhusu Ujenzi wa Kitovu cha Mafuta (Fuel Hub) hapa nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Picha
 

Rais Mhe Samia Suluhu Hassan azungumza katika Mkutano wa Nishati Poweri...

Picha

KITUO CHA ANGA ZANZIBAR YALIKUWA MAFANIKIO MAKUBWA YA WAMAREKANI KWA SAFARI ZA SAYARI

Picha
Kiasi cha kilomita 15 mashariki ya Mji Mkongwe, karibu   ya kijiji cha Tunguu, yapo mabaki yaliyochakaa ya kituo cha Rada cha Kimarekani.   Kituo hiki kilijengwa mwaka 1960 kwa ajili ya kunasia na kuwasiliana na misheni ya mwanzo ya kimarekani ya kwenda angani.   Kituo hichi kilitumika kwa mara ya mwanzo wakati mradi wa mwanzo wa kwenda kwenye Sayari na "Mercury" ulipoanzishwa wakati wanaanga waliporuka katika Parabola yao kutoka Florida kwenda upande mwingine wa Afrika.   Kituo hiki vile vile kipo mlalo wa  nji a y a dunia " Earth track" ya misheni za baadae za mzunguko kwenda kwenye Sayari na kwa hivyo kilikuwa kituo muhimu cha kunasia na pia cha upimaji na upitishaji wa data ambacho kilisaidia kuwasiliana na vyombo hivi vya Angani.  

MBOWE ASEMA TAIFA HILI LINAPASWA KUWA NA WATU AMBAO WAMEUNGANA

Picha

HISTORIA PANA YA ZANZIBAR NA TAWALA MBALI MBALI ZA KIFALME - SAYYID KHALIFA BIN HARUBU

Picha
Jina lake hasa ni Sayyid Khalifa bin Harub bin Thuwein bin Said bin Sultan bin Imam Ahmed bin Said bin Mohammed bin Ahmed bin Khelef bin Said Al Azdy. alizaliwa Oman tarehe 26 mwezi wa Agosti mwaka 1879, mama yake alifariki mudamchache baada ya kujifungua,lipelekwa kulelewa kwenye kasri ya Sultan Sayyid Feisal bin Turki, ambae ndie mjomba wake na ndie alikuwa Sultan wa Muskat.   Alipotimiza miaka 13 alilazimika kuja Unguja kwa babu yake Syd Hemed bin Thuwein, aliyekuwa mfalme wa Zanzibar wakati huo, aliyetawala mwaka 1893 mpaka mwaka 1896 Kwa hivyo yeye ni mjukuu khalisi wa Syd Thuwein, aliyetawala Oman, ambae Mwenyezi Mungu Alimtunukia watoto wengi , akiwemo Syd Harub na Syd Hemed. Na Syd Harub alikufa akiwa kijana sana.  Mama yake aliitwa Turkiya binti Syd Turky bin Said Sultan, Syd Turky ni mtoto wa 5 wa Syd Sutan, ambae aliwahi kutawala Oman mwaka 1871 akafa 1888, ambae ndie baba wa mama yake Syd Khalifa, na akaolewa na Syd Harub na akazaliwa yeye syd Khalifa. Baada ya ku...

HOSPITALI YA KISASA KITOGANI,WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAFUNGULIWA NA RAIS MWINYI

Picha
 Na Mwandishi wetu Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi afungua Hospitali ya  Kisasa ya Kitogani Wilaya ya Kusini  ,Mkoa wa Kusini Unguja. Kufunguliwa kwa Hospitali hii  pia imeambatana na kufungwa kwa  Vifaa tiba vipya,Gari la kubebea wagonjwa,hospitali ipo tayari kutoa huduma tofauti,ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje(OPD),Mama na Mtoto ,huduma za kliniki mbalimbali zikiwemo za Pua,Koo,Masikio ,Macho,Magonjwa yasio ya kuambukiza kama Sukari,shinikizo la damu ,huduma za madawa(pharmacy),huduma za Wagonjwa wanaolazwa ikiwemo ,Wodi za Watoto,Mama Wajawazito kabla na baada ya kujifungua,Watu wazima Wanawake na Wanaume,huduma za wagonjwa wa dharura na ajali,Wagonjwa mahututi(ICU),huduma za watoto njiti ,Wodi tatu za wagonjwa wenye mahitaji maalum ya  kujitenga(isolation) pia Kuna Theatres mbili (2)za kisasa, huduma za ushauri nasaha na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na huduma za uchunguzi ikiwemo Maaba...

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATANGAZA KURUHUSU KUFANYIKA KWA MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.   Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Vyama Vya Siasa 19 waliohudhuria Kikao kilichoitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya Kikao na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Jiji...