HISTORIA PANA YA ZANZIBAR NA TAWALA MBALI MBALI ZA KIFALME - SAYYID KHALIFA BIN HARUBU


Jina lake hasa ni Sayyid Khalifa bin Harub bin Thuwein bin Said bin Sultan bin Imam Ahmed bin Said bin Mohammed bin Ahmed bin Khelef bin Said Al Azdy.
alizaliwa Oman tarehe 26 mwezi wa Agosti mwaka 1879, mama yake alifariki mudamchache baada ya kujifungua,lipelekwa kulelewa kwenye kasri ya Sultan Sayyid Feisal bin Turki, ambae ndie mjomba wake na ndie alikuwa Sultan wa Muskat. 



Alipotimiza miaka 13 alilazimika kuja Unguja kwa babu yake Syd Hemed bin Thuwein, aliyekuwa mfalme wa Zanzibar wakati huo, aliyetawala mwaka 1893 mpaka mwaka 1896
Kwa hivyo yeye ni mjukuu khalisi wa Syd Thuwein, aliyetawala Oman, ambae Mwenyezi Mungu Alimtunukia watoto wengi , akiwemo Syd Harub na Syd
Hemed. Na Syd Harub alikufa akiwa kijana sana. 
Mama yake aliitwa Turkiya binti Syd Turky bin Said Sultan, Syd Turky ni mtoto wa 5 wa Syd Sutan, ambae aliwahi kutawala Oman mwaka 1871 akafa 1888, ambae ndie baba wa mama yake Syd Khalifa, na akaolewa na Syd Harub na akazaliwa yeye syd Khalifa.
Baada ya kufa baba yake Syd Khalifa alilelewa na babu yake Syd Turky na alilelewa pamoja na mjukuu mwengine wa Syd Turky yaani Syd Taimur na walilelewa kishujaa na mafunzo kede kede mpaka akapikika na alipokuja huku Zanzibar akazidi kuwa mahiri na mtaalam wa mengi, hasa  farasi.Siku aliyokuja hakuna
mtu yoyote aliyejuwa aliingia ghafla katika mwaka 1903, na meli aliokuja nayo ikiitwa Aboukir, kabla ya kuja Zanzibar alipitia Makka kwa ajili ya ibada ya Umra, mara ya pili alikwenda na shemeji yake Syd  Ali , na huko ndiko alipokutana na mkewe bi Matuka na wakapendana, ambae naye yeye alifuatana na harimu yake, kaka Ali bin Humud ambae nae pia aliwahi kuwa Sultan wa Zanzibar 
 


Syd Khalifa alifanya mambo mengi ikiwemo  michezo kama ya sailing, polo, tennis na mambo ya kidunia na ya kiakhera [Dini] alimradi  aliishi. Alihudhuria mabaraza mengi sana akiwa 
bado mtoto, kitu kilompelekea kuwa kiongozi mzuri baadae, na kumudu kukaa kwenye kiti cha usultani kwa muda mrefu zaidi. 
Aliowa alipotawala Syd Humud Baada ya kufa Syd Hemed, alimuowa yule yule mpenzi wake Sayyidah Matuka binti Humud, mtoto wa Syd Humud aliyezaa na mkewe Seyyidah Khoufara binti Majid bin Sutan.

Syd Khalifa alipata watoto wawili, baada ya kufa mmoja alizaliwa Syd Prince Sir Abdalla 12 feb 1910. 
na alipokufa Bi Matuka Ndipo alipomuowa Bi Nunuu binti Ahmed. 


Alitawala Zanzibar kuanzia tarehe 9 Disemba mwaka 1911 ,akiwa na miaka 32, ingawa kiti hicho ilikuwa atawale Syd Khalid bin Muhammed, 
lakini Bwana huyu alikataa kata kata kutawala na akajitia maradhi.






Alitawala kwa miaka 49  ni miaka mingi kuliko Sultani yoyote wazanzibar aliepeta kutawala, alifariki Dunia saa 9 alfajiri ya Jumapili ya tarehe 9 Oktober mwaka 1960, sawa sawa na Mwezi 17 Rabil Thani 1380 Hijra. Bwana huyu alikuwa akipendwa mno, kifochake ni moja ya vifo mashuhuri Duniani si Ulaya, si Bara hindi si Afrika wala Uarabuni kila alomfahamu alijuwa kuwa Zanzibar imeondokewa, kwani alikuwa ni mtu wa watu sana.

Wingereza inamtambua kama kiongo mshirika wa vita zoto miili za Dunia dhidi ya Wajerumani,Wamarekani wanamjua alipowaruhusu kujenga kituo kikubwa cha kuongozea safari za Anga pale Tunguu





 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAONESHO YA 6 YA KIMATAIFA YA UTALII YA KISWAHILI (S!TE) YANAFANYIKA KATIKA JIJI LA KIBIASHARA LA TANZANIA LA DAR-ES-SALAAM