MJI WA KILWA KISIWANI ULIVYOBEBA HISTORIA YA MATAIFA MBALIMBALI


 Katika kisiwa cha Kilwa kuna wakati ilikuwa dola inayojitawala na kusifika kwa utajiri,eneo hilo ni mji katika mkoa wa Lindi ulioko kusini mwa Tanzania.





Kilwa kisiwani ni mji unaopatikana katika fukwe za Bahari ya Hindi, Kusini mwa Tanzania. Ni mji ulioorodheshwa katika urithi wa Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Hili limetokana na ukongwe wa mji wa Kilwa kisiwani ambao ulifahamika hata kabla ya karne ya 9 kwani katika jengo la Ngome ya Mreno lijulikanalo kama gereza pameandikwa mwaka 230 juu ya mlango kuashiria kujengwa kwa jengo hilo 

Jina la Mji wa Kilwa lilitokana na neno la Kirumi Qviloa ambalo wenyeji walishindwa kutamka na kuita kwa jina la Kilwa, Mji huu ulikuwa ni himaya muhimu ya kibiashara katika bahari ya hindi ikiwa na umaarufu katika biashara za utumwa, chumvi, meno ya tembo na dhahabu. 

Biashara hizi zilivutia himaya hii kuwa na sarafu yake na utawala wenyewe nguvu wakisultan.Eneo hili lilitembelewa na watu wengi maarufu duniani akiwemo mfanyabiashara maarufu Ibn Battuta kutoka Moroco na Vasco Da gama kutoka Ureno ambaye alijenga himaya yake katika mji huu 

Mpaka sasa mji huo unaendelea kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi wanaofika kushuhudia magofu ya majengo ya zamani, misikiti zaidi ya 90 ukiwemo msikiti mkongwe na mkubwa Afrika Mashariki na Kati uliojengwa tangu karne ya tisa.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii