HOSPITALI YA KISASA KITOGANI,WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAFUNGULIWA NA RAIS MWINYI
Na Mwandishi wetu Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi afungua Hospitali ya Kisasa ya Kitogani Wilaya ya Kusini ,Mkoa wa Kusini Unguja.
Kufunguliwa kwa Hospitali hii pia imeambatana na kufungwa kwa Vifaa tiba vipya,Gari la kubebea wagonjwa,hospitali ipo tayari kutoa huduma tofauti,ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje(OPD),Mama na Mtoto ,huduma za kliniki mbalimbali zikiwemo za Pua,Koo,Masikio ,Macho,Magonjwa yasio ya kuambukiza kama Sukari,shinikizo la damu ,huduma za madawa(pharmacy),huduma za Wagonjwa wanaolazwa ikiwemo ,Wodi za Watoto,Mama Wajawazito kabla na baada ya kujifungua,Watu wazima Wanawake na Wanaume,huduma za wagonjwa wa dharura na ajali,Wagonjwa mahututi(ICU),huduma za watoto njiti ,Wodi tatu za wagonjwa wenye mahitaji maalum ya kujitenga(isolation) pia Kuna Theatres mbili (2)za kisasa, huduma za ushauri nasaha na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na huduma za uchunguzi ikiwemo Maabara ,Ultrasound,ECG na XRAYS.Kuna huduma za kisasa za Mfumo wa Tehama zikiwemo huduma za data,sauti na picha zitakazotumika katika kutoa elimu ya afya kwa wagonjwa na wananchi wanaofika katika hospitali hii,usajili wa mahudhurio ya wafanyakazi ,mifumo ya tahadhari ya moto ,Mfumo wa Nursing call System na Mfumo wa kutunza taarifa za wagonjwa kieletroniki(EMR).
Hospitali itawahudumia Wananchi zaidi ya 52,850 wakaazi wa Wilaya ya Kusini na maeneo jirani,
Maoni
Chapisha Maoni