K atika kisiwa cha Kilwa kuna wakati ilikuwa dola inayojitawala na kusifika kwa utajiri,eneo hilo ni mji katika mkoa wa Lindi ulioko kusini mwa Tanzania. Kilwa kisiwani ni mji unaopatikana katika fukwe za Bahari ya Hindi, Kusini mwa Tanzania. Ni mji ulioorodheshwa katika urithi wa Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Hili limetokana na ukongwe wa mji wa Kilwa kisiwani ambao ulifahamika hata kabla ya karne ya 9 kwani katika jengo la Ngome ya Mreno lijulikanalo kama gereza pameandikwa mwaka 230 juu ya mlango kuashiria kujengwa kwa jengo hilo J ina la Mji wa Kilwa lilitokana na neno la Kirumi Qviloa ambalo wenyeji walishindwa kutamka na kuita kwa jina la Kilwa, Mji huu ulikuwa ni himaya muhimu ya kibiashara katika bahari ya hindi ikiwa na umaarufu katika biashara za utumwa, chumvi, meno ya tembo na dhahabu. Biashara hizi zilivutia himaya hii kuwa na sarafu yake na utawala wenyewe nguvu wakisultan. Eneo hili lilitembelewa na watu we...
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Philip Morris, Gregoire Verdeaux na Ujumbe wake walipofika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Philip Morris, Gregoire Verdeaux na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023
Katika kijiji cha Paje Mjogooni, Unguja – Zanzibar, Mama Shemsa John Taraba ameibuka kama mfano bora wa mwanamke mjasiriamali aliyegeuza changamoto kuwa fursa kupitia ufugaji wa kuku wa mayai. Kupitia juhudi zake, ameonyesha kuwa kilimo na ufugaji si kazi ya wanaume pekee, bali ni nyenzo ya kiuchumi kwa kila Mtanzania mwenye maono na dhamira ya kufanikisha ndoto zake. Safari ya Mama Shemsa ilianza kwa kuku 830 pekee, akizalisha tray 36 za mayai kwa siku. Kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kupitia mkopo nafuu na ushauri wa kitaalamu, alijipatia ujuzi na mtaji uliomuwezesha kufanya mageuzi makubwa. Leo hii, anafuga kuku 5,000 wanaozalisha wastani wa tray 145 kwa siku – huku soko likibaki na kiu ya zaidi ya uzalishaji wake. Mafanikio ya Mama Shemsa yameacha alama kubwa kijijini na Zanzibar kwa ujumla: Mahitaji makubwa ya bidhaa – mayai yake yanauzwa kabla hata hayajazalishwa. Ajira kwa jamii – amewaajiri vijana na wanawake wa Paje, na kuongeza k...
Maoni
Chapisha Maoni