KITUO CHA ANGA ZANZIBAR YALIKUWA MAFANIKIO MAKUBWA YA WAMAREKANI KWA SAFARI ZA SAYARI

Kiasi cha kilomita 15 mashariki ya Mji Mkongwe, karibu ya kijiji cha Tunguu, yapo mabaki yaliyochakaa ya kituo cha Rada cha Kimarekani. Kituo hiki kilijengwa mwaka 1960 kwa ajili ya kunasia na kuwasiliana na misheni ya mwanzo ya kimarekani ya kwenda angani. Kituo hichi kilitumika kwa mara ya mwanzo wakati mradi wa mwanzo wa kwenda kwenye Sayari na "Mercury" ulipoanzishwa wakati wanaanga waliporuka katika Parabola yao kutoka Florida kwenda upande mwingine wa Afrika. Kituo hiki vile vile kipo mlalo wa njia yadunia" Earth track" ya misheni za baadae za mzunguko kwenda kwenye Sayari na kwa hivyo kilikuwa kituo muhimu cha kunasia na pia cha upimaji na upitishaji wa data ambacho kilisaidia kuwasiliana na vyombo hivi vya Angani.




 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii