MAVUNDE: UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UJENZI WA MABWAWA YA UMWAGILIAJI ITACHOCHEA KUKUA KWA SEKTA YA KILIMO
Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa An thony Mavunde amesema utekelezaji wa miradi ya mabwawa unaoendelea nchini hivi sasa utasaidia sana kukuza sekta ya kilimo nchini Tanzania na kuongeza eneo kubwa zaidi linalofanya kilimo cha umwagiliaji. Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 12 Novemba, 2022 wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa bwawa la Membe linalojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma. "Katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali kupitia Tume ya Umwagiliaji imepanga kujenga jumla ya mabwawa 14 nchi nzima, likiwemo bwawa hili la Membe litakalo kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita Bilioni 12. Pamoja na bwawa hili kutumika katika shughuli za umwagiliaji, pia litawekwa miundombinu ya kusaidia unyweshaji maji mifugo, kupeleka maji ya matumizi ya majumbani kwa vijiji vinavyozunguka na kuwa sehemu ya utalii kwa wananchi mbalimbali, hatua ambayo itaongeza mapato ya Halmashauri ya Chamwino. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametuongezea bajeti Wizara ya Kilimo ambapo fedha nyingi zimee...