ASILIMIA 40 YA WATU DUNIANI WANAKABILIWA NA UHABA WA MAJI
Mtu mmoja kati ya wanne wataishi katika nchi ambako ukosefu wa maji utakuwa ni tatizo sugu na linalojirudia ifikapo mwaka 2050.
maji salama na usafi kwa wote ambalo ni lengo namba 6 la SDG’s ni muhimu katika kutimiza malengo mengine, na linachangia katika kupunguza umasikini, kukuza uchumi na kuwa na mifumo bora ya maisha.
Hatuwezi kuichukulia amani au rasilimali ya thamani ya maji kimzaha. Kwani kwa hakika maji ni suala la uzima na mauati, miili yetu asilimia 60 ni maji. Miji yetu, viwanda vyetu na kilimo chetu vyote vinayategemea rasilimali hiyo.”
Kote duniani hivi sasa zaidi ya watu bilioni mbili hawana fursa ya kupata maji salama na zaidi ya bilioni 4.5 hawana huduma za kutosha za usafi na kujisafi.
Maoni
Chapisha Maoni