Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI, NEMBO YA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NA MFUMO RASMI WA OFISI HIYO KATIKA MKUTANO MKUU WA MAWAKILI WA SERIKALI JIJINI DODOMA TAREHE 29 SEPTEMBA, 2022

Picha
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 29 Septemba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujionea shughuli mbalimbali pamoja na huduma zitolewazo na Ofisi hizo kabla ya kuhutubia na kuzindua Rasmi Chama cha Mawakili wa Serikali, nembo na Mfumo rasmi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kwenye  laptop  kuzindua mfumo rasmi wa Kieletroniki wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAGMIS), nembo  ya Ofisi hiyo pamoja na Chama cha Mawakili wa Serikali katika Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali uliofanyika kw

SERIKALI IMETENGA BIL 100 UJENZI WA VETA NCHINI-WAZIRI MKENDA

Picha
Na Mathias Canal, WEST-Dodoma Serikali inayo azma ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka huu wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni Mia moja (100 Bil). Kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa Wilaya ambazo zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi. Aidha, Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Wilaya hizo 62 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda amesema hayo leo tarehe 21 Septemba 2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Jimbo Manyoni Mashariki aliyetaka kufahamu serikali ina Mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Wilayani Manyoni Waziri Mkenda amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha 2022/23, Serikali imetenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi katika Wilaya 62 kwa

SERIKALI IMEWEKEZA KATIKA CHUO CHA USAFIRISHAJI (NIT) KUTOKANA NA MIRADI YA KIMKAKATI, KWA SASA UHANDISI WA MELI,NDEGE,UMEME WA TRENI YA KISASA,URUBANI NA UHUDUMU WA NDEGE TUNAJIVUNIA KUPATIKANA HAPA TANZANIA

Picha
Darasa lenye vifaa vya kisasa vya kufundishia mwanzo kushoto ni mguu wa Ndege,inafuata sehemu ya Mifumo ya hewa Ama hydroric Mjini ya pesto na mwisho ni Mifumo es GT Stoo ya Spana na vitu vyote vinavyowezesha  kazi ya Ufundi kuimarika Hii ndio JET enjini Tulizo Chusi Afisa Habari wa NIT akifafanua jambo kwa  mkuu  wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa, Baadhi ya Magari yanayotumika kwa kufundishia udereva Vijana wa mwaka wa 3 uhandisi wa Ndege wakimsikiliza kwa making Mwalimu wao Piton Injini Jet injini Chumba maalumu kwa mafunzo ya uhandisi wa ndege Chumba cha kisasa kwa ajili ya mafunzo ya urubani Vifaa vya kisasa katika karakana ya ubaguzi wa magari Wahandisi wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa uhadisi wa ndege Wanafunzi wakwanza kujifunza Uhandisi wa Umeme wa Treni Wanafunzi wa mwaka wa pili koi ya uhandisi wa ndege MKUU wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa, a m e m s h u k u r u Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukiongezea chuo

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI NCHINI WINGEREZA KUHUDHURIA MAZISHI YA MALKIA ELIZABETH II

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na muwakilishi wa Mfalme Charles III, Bi. Cynthia Gresham wa Uingereza pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo, Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Luton tarehe 17 Septemba, 2022 kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II wa Uingereza yatakayofanyika tarehe 19 Septemba, 2022 jijini London.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN ALI MWINYI AZINDUA RIPOTI YA MAHITAJI YA MAHAKAMA ZANZIBAR NA UZINDUZI WA OFISI ZA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU ZANZIBAR KATIKA UKUMBI WA GOLDEN TULIP ZANZIBAR

Picha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika hafla ya Uzinduzi wa Ripoti ya Mahitaji ya Mfumo wa Mahakama Zanzibar na Uzinduzi wa Ofisi ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Zanzibar, uzinduzi huo uliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja  tarehe 17-9-2022.(Picha na Ikulu)  

ZIARA YA RC MOROGORO YAUKATAA MRADI WA BARABARA MOROGORO VIJIJINI

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Fatma Mwassa amekataa Mradi wa Barabara ya Zege iliyojengwa Chini ya kiwango , katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kata ya Matombo barabara ya Kigongo Juu . Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa amemuagiza Katibu tawala wa Mkoa docta Mussa pamoja na Engineer wa Mkoa kumsimamia Mkandarasi kurudia kumwaga zege Upya .  Mkuu wa Mkoa yupo kwenye ziara yake ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kuzunguka Mkoa wa Morogoro na Halmashauri zake zote na leo alikuwa Halmshauri ya Morogoro.

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM TANZANIA BARA NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AMESAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KUFUATIA KIFO CHA MALKIA ELIZABETH II

Picha

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA RAIS WA JAMHURI YA KENYA DKT. WILLIAM SAMOEI RUTO, NAIROBI NCHINI KENYA

Picha

MAPITIO YA SERA NA MITAALA YANAANGAZIA PIA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA-WAZIRI MKENDA

Picha
Na Mathias Canal, WEST-Morogoro   Serikali imesema kuwa inaendelea kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala ili kuongeza ubora wa elimu na mafunzo.   Katika Mapitio hayo ya mitaala na sera pia yanaangazia kwa karibu Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ili wakati utatuzi wa changamoto ukiendelea serikali kuangalia nini kifanyike ili kuboresha elimu ujuzi kwa wanafunzi ikiwemo watu wazima.   Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 9 Septemba 2022 wakati wa hafla fupi ya ufungaji wa mafunzo ya Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya elimu ya watu wazima (TEWW) Kampasi ya Morogoro.   Prof Mkenda amesema kuwa Taasisi hiyo inapaswa kushiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni ikiwa ni pamoja na kushirikisha kwa karibu wadau wengine kutoa maoni namna ya kuboresha taasisi hiyo hususani katika maeneo ya ujuzi.   Pia, Prof Mkenda amesema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatekeleza mael