SERIKALI IMEWEKEZA KATIKA CHUO CHA USAFIRISHAJI (NIT) KUTOKANA NA MIRADI YA KIMKAKATI, KWA SASA UHANDISI WA MELI,NDEGE,UMEME WA TRENI YA KISASA,URUBANI NA UHUDUMU WA NDEGE TUNAJIVUNIA KUPATIKANA HAPA TANZANIA
Darasa lenye vifaa vya kisasa vya kufundishia mwanzo kushoto ni mguu wa Ndege,inafuata sehemu ya Mifumo ya hewa Ama hydroric Mjini ya pesto na mwisho ni Mifumo es GT |
Stoo ya Spana na vitu vyote vinavyowezesha kazi ya Ufundi kuimarika |
Hii ndio JET enjini |
Tulizo Chusi Afisa Habari wa NIT akifafanua jambo kwa mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa, |
Baadhi ya Magari yanayotumika kwa kufundishia udereva |
Vijana wa mwaka wa 3 uhandisi wa Ndege wakimsikiliza kwa making Mwalimu wao |
Piton Injini |
Jet injini |
Chumba maalumu kwa mafunzo ya uhandisi wa ndege |
Chumba cha kisasa kwa ajili ya mafunzo ya urubani |
Vifaa vya kisasa katika karakana ya ubaguzi wa magari |
Wahandisi wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa uhadisi wa ndege |
Wanafunzi wakwanza kujifunza Uhandisi wa Umeme wa Treni |
Wanafunzi wa mwaka wa pili koi ya uhandisi wa ndege |
MKUU wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa, a m e m s h u k u r u Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukiongezea chuo hicho uwezo wa kifedha na kufanya kizidi kuimarika katika utendaji.
Amesema kwamba kufuatia Serikali ya Awamu ya Sita kukiwezesha chuo hicho kifedha, matunda yake sasa yameanza kuonekana kwa kuongeza kasi ya kuzalisha wataalamu wa reli, meli, bandari na anga.
Kwa mujibu wa Profesa Mganilwa, NIT mbali ya kufundisha kozi kongwe za udereva wa magari, masoko na mawasiliano ya umma, utawala na nyinginezo, pia chuo hicho kimekuwa kinawanoa wasanifu, wahandisi na wasimamizi wa meli, ndege na bandari na kozi ya urubani.
Anasema mojawapo ya mafanikio makubwa waliyopata chini ya serikali ya Rais Samia ni NIT kuwezeshwa kununua ndege mbili mpya zenye thamani ya sh. bilioni 1.2 kwa kila moja.
Uongozi wa NIT umelipa fedha kwa ajili ya kununua kifaa cha kufundishia wahudumu ndani ya ndege (mock-up), ambapo uwezo huo umetokana na serikali ya awamu ya sita kukipa chuo hicho fedha za kukidhi mahitaji yote muhimu.
“Rais (Samia) ametupatia fedha na tumeshalipa gharama ya hizo ndege,Profesa Mganilwa anasema baada ya serikali kukiwezesha kifedha chuo cha NIT, hatimaye kimefanikiwa kupeleka nje ya nchi wataalamu wake zaidi ya 65 ili kusomea ujuzi mbalimbali na mpango uliopo baadaye ni kupeleka katika vyuo vya nje wataalamu zaidi nia ikiwa kuhakikisha wataalamu hao wanaongezewa ujuzi.
MIRADI MIKUBWA,NA HALI YA AMANI
Profesa Mganilwa anampongeza Rais Samia kwa kuendelea kukamilisha ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati huku nchi ikiwa katika utulivu wa hali ya juu.
“Tumeendelea kuwa na utulivu pia ‘so far’ hatujawa na masuala ya uvunjifu wa amani na vile vile hatujakumbwa na baa la njaa kwa hiyo majanga haya mwenyezi Mungu anatusaidia hayajatukuta,” anaeleza sehemu ya mafanikio hayo ya serikali ya awamu ya sita.
Profesa Mganilwa anasema Tanzania inakwenda vizuri kutokana na mambo yaliyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025 kuwa katika hatua ya utekelezaji na miradi kadhaa imekuwa inaelekea kukamilika.
Serikali ya awamu ya sita nchi imekuwa haina baa la njaa na hali ya amani na utulivu imetawala kwa kiasi kikubwa na kuwafanya Watanzania waendelee kufanya shughuli zao bila ya hofu yoyote.
“Nishukuru kwanza kwa sababu vitu vingi walivipanga maana yake walitengeneza Ilani ya Uchaguzi (ya 2020-2025) na yeye alishiriki kuitengeneza ambayo ndio inatekelezwa na alizunguka nchi nzima kipindi kile kuitafsiri kwa wananchi wawapigie kura,” anasema.
Profesa Mganilwa anaongeza: “Tunakwenda vizuri kwa sababu sijaona yale waliyoahidi kuyatekeleza kwa wananchi sijaona hata moja tukasema hili tume-cancel (tumefuta), hili tumeshindwa, kwa hiyo karibu yote yanaendelea vizuri.”
“So far (mpaka sasa) sijaona kilichosimama kwa sababu SGR (reli ya kisasa) inaendelea, ununuzi wa ndege unaendelea, blue economy (uchumi wa bluu) humo ndio ilikuwa Ilani pekee ambayo imeipa umuhimu sana na inaendelea kutekelezwa,” anasema Profesa Mganilwa.
Maoni
Chapisha Maoni