ZIARA YA RC MOROGORO YAUKATAA MRADI WA BARABARA MOROGORO VIJIJINI
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Fatma Mwassa amekataa Mradi wa Barabara ya Zege iliyojengwa Chini ya kiwango , katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kata ya Matombo barabara ya Kigongo Juu . Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa amemuagiza Katibu tawala wa Mkoa docta Mussa pamoja na Engineer wa Mkoa kumsimamia Mkandarasi kurudia kumwaga zege Upya . Mkuu wa Mkoa yupo kwenye ziara yake ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kuzunguka Mkoa wa Morogoro na Halmashauri zake zote na leo alikuwa Halmshauri ya Morogoro.
Maoni
Chapisha Maoni