|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto), akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofikia kilele leo katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. Kulia ni Katibu Muhtasi wa Wizara hiyo, Bi. Masia Msuya |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto), akisikiliza kwa umakini maelezo yaliyokuwa yanaotolewa na Mchumi kutoka Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bi. Gloria Mduda (kulia), kuhusu mwamko wa wananchi waliotembelea meza ya idara hiyo, kujifunza kuhusu Deni la Taifa, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofikia kilele leo katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”.
|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kulia), akimsikiliza kwa umakini, Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha Bi. Mary Mihigo (katikati), kuhusu namna idara hiyo ilivyotoa elimu ya fedha kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofikia kilele leo katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. Kushoto ni Mchumi, Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bw. Joseph Msumule. |
|
Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Bi. Theresia Mendoza (kushoto), akielezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho, kwa Mwananchi aliyetembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayohitimishwa leo katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. |
Mtaalamu kutoka Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Bw. George Killo (Kushoto), akitoa elimu kuhusu Mfumo wa Kusajili Madalali (GAMIS), kwa wananchi waliotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”.
|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto), akisikiliza kwa umakini maelezo yaliyokuwa yanaotolewa na Afisa Uhusiano kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Bi. Stella Kalinga (katikati), kuhusu mwamko wa wananchi waliotembelea Banda la Chuo hicho, kujua utaratibu na kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo hicho, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofikia kilele chake leo katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. Kulia ni Afisa Uhusiano, Bw. Dennis Mlay. |
|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa pili kushoto), akisikiliza kwa umakini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mratibu wa Mradi wa Maziwa (TI3P) wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Bw. Joseph Mabula (wa kwanza Kulia), ambapo ameeleza jinis mradi huo unavyowanufaisha wafugaji nchini, alipotembelea Banda la Taasisi hiyo iliyo chini ya Wizara ya Fedha, katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, katika viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa TADB, Bw. Waziri Mkani (wa pili kulia), Meneja Mawasiliano na Masoko, Bw. Amani Nkurlu (katikati) na Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Benki hiyo Bw. Mike Granta (wa kwanza kushoto). |
|
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Fedha, baada ya kutembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. |
Maoni
Chapisha Maoni