BANDA LA WIZARA YA FEDHA: SHAMRASHAMRA ZA MAADHIMISHO YA SIKU YA NANE NANE JIJINI MBEYA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto), akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofikia kilele leo katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. Kulia ni Katibu Muhtasi wa Wizara hiyo, Bi. Masia Msuya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (kushoto), akisikiliza kwa umakini maelezo yaliyokuwa yanaotolewa na Mchumi kutoka Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bi. Gloria Mduda (kulia), kuhusu mwamko wa wananchi waliotembelea meza ya idara hiyo, kujifunza kuhusu Deni la Taifa, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane, yanayofikia kilele leo katika Viwanja vya John Mwakangale, jijini Mbeya, yaliyobeba kaulimbiu ya “Vijana na Wanawake ndio Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula Tanzania”. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ...