MBUNGE wa Bunge la Uingereza, Tracey Crouch anaendelea kupanda Mlima Kilimanjaro

  



MBUNGE wa Bunge la Uingereza, Tracey Crouch anaendelea kupanda Mlima Kilimanjaro na Jana amefika kituo cha Moyr Hut mita takriban 4,600 kutoka usawa wa bahari akibakiza vituo vitatu kufika kileleni na kuweka historia . Crouch anapanda Mlima Kilimanjaro, akiwa na wanawake wenzake wanane kupitia kampuni ya Big Expedition and Safaris ya jijini Arusha na tangu ameanza kupanda amekuwa na furaha kubwa kupanda Mlima huku akifurahia kukaribia kileleni mwa Mlima Kilimanjaro. Mbunge huyo ambaye yupo katika kampeni ya kuchangisha fedha kufanikisha matibabu ya saratani ya matiti kwa wagonjwa kesho anatarajiwa kufika kituo cha Baranko. Crouch ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Michezo wa Uingereza kati ya mwaka 2017/18 anatarajiwa kushuka Mlimani Agosti 5 na kupokewa na wadau mbalimbali wa Utalii kampuni ya kimataifa ya Utalii ya Uingereza ya Action Challenge kwa kushirikiana na Big Expedition and Safaris ndio wanampandisha kileleni Mbunge huyo na wenzake katika safari iliyopewa jina la Delux VIP ambapo wanaopanda mlima wanapewa huduma za viwango vya juu zaidi (VIP service). Mbunge huyo, ameanza Julai 29,2023 kupanda mlima huo mrefu barani Afrika, kupitia njia ya Lemosho .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAONESHO YA 6 YA KIMATAIFA YA UTALII YA KISWAHILI (S!TE) YANAFANYIKA KATIKA JIJI LA KIBIASHARA LA TANZANIA LA DAR-ES-SALAAM