RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.HUSSEIN ALI MWINYI AFUNGUA MAONESHO YA SIKU 3 YA UTALII NA UWEKEZAJI ZANZIBAR 2023
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kwa dhati kuiendeleza sekta ya Utalii na kuongeza thamani na ubora kwa kutumia mikakati tofauti ikiwemo kuongeza vivutio.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua Maonesho ya siku 3 ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar 2023 yenye washiriki zaidi ya 200 kutoka Mataifa mbalimbali duniani.
Maonesho hayo yenye maudhui ya 'Greener Zanzibar' ambayo yanalenga kuibadilisha Zanzibar kuwa fikio la utalii endelevu, yaani 'Sustainable Tourism Destination'
๐ 09 Februari 2023,
๐ Jengo la Kihistoria la Beit El Amaan, Zanzibar
Maoni
Chapisha Maoni