RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA KIKWETE, MWENYEKITI WA BODI YA TAASISI YA KIMATAIFA INAYOSHUGHULIKIA MASUALA YA ELIMU DUNIANI (GLOBAL PARTNERSHIP FOR EDUCATION) - GPE) AMEKUTANA NAKUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA BENKI YA DUNIA WASHINGTON DC




Viongozi wa Benki ya Dunia aliokutana nao ni Bi. Mari Pangetsu, Mkurugenzi Mtendaji wa Sera ya Maendeleo na Ushirikiano wa Benki ya Dunia, na Bi. Mamta Murthi, Makamu wa Rais wa Maendeleo ya Watu katika Benki ya Dunia.
Kutoka GPE Mwenyekiti wa Bodi Dr. Jakaya Kikwete aliambana na Bi. Laura Frigenti, Mtendaji Mkuu wa GPE na Bw. Charles North, Naibu Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.
Mkutano huo ulilenga katika kuboresha ushirikiano uliopo kati ya GPE na Benki ya Dunia katika kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa watoto wa kike na wa kiume katika nchi zinazoendelea.
📸:O/Rais Mstaafu

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii