Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema Wizara hiyo imeanza usajili wa Wakulima kwa mwezi mmoja sasa na wamefikia takribani Wakulima Milioni 1.3 kwenye mfumo na 50% wamepata namba zao za siri na namba maalumu (unique identity number).
 |
| Wakulima wengi wenye umri mdogo ni wanawake, na sasa tunaona ongezeko la wakulima wenye mashamba yenye ukubwa wa hekari 5 hadi 50.
Ukodishaji wa mashamba umeanza kuonekana umeongezeka kwenye mashamba makubwa kuanzia hekari 10-300. |
 |
| wakulima wengi waliosajiliwa wana utambulisho (NIDA), taswira inaonyesha zaidi ya asilimia 70 wana umri wa kati 18-50yrs ,kwamba ile dhana kuwa kilimo kimetawaliwa na mababu inaonekana kuwa sio sahihi. |
Maoni
Chapisha Maoni