HAFLA YA CHAKULA CHA MCHANA NA SERENGETI GIRLS

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  Julai 05, 2022 Ikulu Dar es Salaam ameikaribisha Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake chini ya Umri wa Miaka 17 ( Serengeti Girls)  chakula cha mchana ikiwa ni muendelezo wa pongezi zake kwa  timu hiyo baada ya Kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini India.

Viongozi wa Serikali na Mpira wa Miguu  wakiongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbas  na wengine wamehudhuria tukio hilo.

Hafla hiyo, imepambwa na Wasanii mbalimbali wa Muziki wa kizazi kipya akiwemo Barnaba na Frida Amani.

















  

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MJI WA KILWA KISIWANI ULIVYOBEBA HISTORIA YA MATAIFA MBALIMBALI

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA PHILIP MORRIS GREGOIRE VERDEAUX IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA