Machapisho

MAPITIO YA SERA NA MITAALA YANAANGAZIA PIA TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA-WAZIRI MKENDA

Picha
Na Mathias Canal, WEST-Morogoro   Serikali imesema kuwa inaendelea kufanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala ili kuongeza ubora wa elimu na mafunzo.   Katika Mapitio hayo ya mitaala na sera pia yanaangazia kwa karibu Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ili wakati utatuzi wa changamoto ukiendelea serikali kuangalia nini kifanyike ili kuboresha elimu ujuzi kwa wanafunzi ikiwemo watu wazima.   Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 9 Septemba 2022 wakati wa hafla fupi ya ufungaji wa mafunzo ya Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya elimu ya watu wazima (TEWW) Kampasi ya Morogoro.   Prof Mkenda amesema kuwa Taasisi hiyo inapaswa kushiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni ikiwa ni pamoja na kushirikisha kwa karibu wadau wengine kutoa maoni namna ya kuboresha taasisi hiyo hususani katika maeneo ya ujuzi.   Pia, Prof Mkenda amesema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tek...

EWURA INATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA BOMBA LA EACOP

Picha
Menejimenti ya EWURA na ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mafuta Uganda (PAU) wakiwa Eneo Huru (No man’s Land) katika mpaka wa Tanzania na Uganda (Mutukula) eneo liltakapo pita bomba la kusafirisha mafuta ghafi kwenda Chongoliani, Tanga, Tarehe 15.8.2022 Timu ya EWURA eneo litakalopita Bomba kutoka Uganda kwenda Tanga. Hapa ni Kyaka- Misenyi Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Martin Tiffen akionyesha Ramani Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Modestus Lumato Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Martin Tiffen( wa pili kushoto) akionesha Timu ya EWURA eneo litakalopita Bomba kutoka Uganda kwenda Tanga. Hapa ni Kyaka- Misenyi  

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MKOANI IRINGA

Picha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Wananchi wa Mkoa wa Iringa alipowasili katika Uwanja wa CCM Samora kwa ajili ya kuhutubia Mkutano wa Hadhara tarehe 12 Agosti, 2022.    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Iringa kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa CCM Samora tarehe 12 Agosti, 2022.  

OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI ZINGATIENI MASLAHI MAPANA YA NCHI

Picha
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb) akizungumza na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (hawapo pichani) wakati wa kikao chake cha kujadili utekelezaji wa majukumu ya Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (aliyevaa miwani) wakati wa kikao cha Waziri huyo na Menejimenti ya Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb) (aliyesimama mbele katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kikao kazi na Ofisi hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro (aliyeketi mbele meza kuu) wakati wa kikao cha kuj...

WIZARA YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA EXTENSIA YA UINGEREZA

Picha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama  Connect To Connect,  tukio lililofanyika  Julai 25, 2022 jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama  Connect To Connect.  Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara hiyo, Bi. Lugano Rwetaka.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Ma...

MAKAMU WA RAIS MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA DORIS MOLLEL FOUNDATION JULAI 25

Picha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 25 Julai 2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, mara baada ya Mazungumzo yaliofanyika Jijini  Dar es salaam  tarehe 25 Julai 2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango  tarehe 25 Julai 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, Mazungumzo yaliofanyika Jijini...