Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2024
Picha
  MKUTANO WA 16 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA NISHATI WA AFRIKA MASHARIKI WAANZA JIJINI ARUSHA Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umenza leo tarehe 12 Februari 2024 katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.    Mkutano huo wa siku tatu kuanzia February 12 hadi 14, 2024 utafanyika katika ngazi tatu; ngazi ya Wataalamu tarehe 12 Februari 2024, ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 13 Februari 2024 na kuhitimishwa katika ngazi ya Mawaziri tarehe 14 Februari 2024.     Mkutano huo unatarajiwa kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nishati katika Jumuiya. Vilevile kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua chagamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika na endelevu katika Jumuiya.    Maeneo ya sekta ya nishati yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni; umeme, mafuta na nishati jadidifu.  Awali akizungumza kwenye ufunguzi wa m...