JE UNAJUA DELTA YA RUFIJI NDIO ENEO ZIMEZAMISHWA MELI KUBWA MBILI ZA KIVITA ZA UJERUMANI? SEHEMU YA NNE
Baada ya vita vya Rufiji Delta Wanamaji wanajeshi 188 waliobaki waliwazika Wajerumani wenzao 33 wengi walikufa kwa homa kali na mashambulizi siku iliyofuata. Kibao chenye maneno “Beim Untergang S.M.S. Königsberg am 11.7.15 gefallen…” ikimaanisha (“Aliuawa vitani wakati SMS Königsberg ilipozamishwa Julai 11 1915…” iliwekwa, pamoja na orodha ya waliokufa. Bunduki kumi za inchi 4.1 (milimita 105) za kurusha risasi haraka haraka. zilizopatikana kutoka Königsberg ziliwekwa kwenye matoroli ya ardhini na kuwekwa kama bunduki za kutisha zenye ufanisi wa ajabu katika vita vya msituni vya Wajerumani dhidi ya washirika wao katika Afrika Mashariki. Mizinga hiyo ilitumika jijini Dar es Salaam kama ngome ya bandari, huku moja ikiwekwa kwenye Graf von Götzen, meli ya abiria ambayo ndio Mv liemba ya leo iliyoko ziwa Tanganyika. Haikuwa hadi Oktoba ya 1917 kwamba bunduki ya mwisho ilipigwa nje. Wanajeshi wengine wa Königsberg walijiunga na vikosi vya ardhini vilivyoamriwa na Lettow-Vorbeck...